Takwimu kuhusiana na Corona bara la Afrika hii leo

who
who
NA NICKSON TOSI

Mataifa zaidi ya 50 katika bara la Afrika kufikia sasa yamedhibitisha visa mbalimbali vya maambukizi ya Corona ambayo yameathiri mataifa mengine Ulimwenguni.

Hapa tumekudokolea idadi ya visa vya maambukizi katika matiafa ya Afrika japo takwimu hizi hubadilika kila mara kutokana na visa vingi vya maambukizi ambavyo mataifa mbalimbali yanaendelea kuripoti.

Jedwali lifuatalo limetoa hali halisia ya visa vya Corona kulingana na shirika la Afya duniani WHO tawi la Afrika.

Kutoka kwa jedwali hilo Afrika kusini ingali inaongoza kwa visa vya maambukizi vikiwa 1934, huku taifa la Algeria likiongoza kwa idadi kubwa ya watu walioaga dunia ikiwa 235.

Katika Ukanda wa Afrika Mashariki Kenya ingali kidedeani na visa 189 vya watu walioambukizwa huku watu waliopoteza maisha yao ikiwa 7 na waliopata nafuu ikiwa 22.

Mataifa ya Burundi na Sudan Kusin ndiyo ya kipekee katika bara la Afrika ambayo yamesejali visa vichache mno ,vikiwa 3 kwa kila taifa.

Fahamu kuwa takwimu hizo zimetolewa chini ya masaa 24, na huenda zikabadilika kadri muda unavyosonga .