TANZIA: Watu 7 wafariki katika ajali mbaya ya barabara eneo la Turbo

Watu saba walifariki katika ajali ya barabara katika eneo la Turbo kwenye barabara ya Eldoret - Webuye, baada ya matatu walimokuwa wakisafiria kugongana na trela.

Wengine kadhaa walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Moi. Matatu hiyo iliharibika vibaya.

Matatu hiyo ilikuwa ikielekea Webuye huku trela ikielekea eneo la Eldoret. Walioshuhudia walisema kuwa gari moja kati ya hayo mawili lilikuwa likipitia upande usiofaa katika daraja na kusababisha ajali hiyo.

Afisa mkuu wa polisi katika kaunti ya Uasin Gishu Johnstonne Ipara alithibitisha ajali hiyo na kusema kwamba wengi wa majeruhi walikuwa katika hali mbaya.

-Mathews Ndanyi