Tanzia!Mwimbaji wa Ohangla Lady Mareen Ameaga

Lady-maureen-3
Lady-maureen-3
Wasanii,jamaa na marafiki hii leo wameamka na kupata habari za huzuni kuwa Msanii wa nyimbo za ohangla Lady Maureen almaarufu Maureen Achieng alipumua pumzi yake ya mwisho mnamo saa tisa alfajiri jumamosi.

Msanii Maureen amekuwa mgonjwa kwa muda wa miaka miwili sasa, huku akilazwa hospitali na kutoka, aliaga dunia akiwa katika kaunti ya Migori.

Kifo chake kilitangazwa na msanii wa nyimbo za Rhumba Wuod Fibi huu hapa ujumbe wake,

"Tumepoteza shujaa mwingine,pigo kubwa kwa tasnia ya usanii na kenya kwa jumla, lala pahali pema Lady Maureen

Nilikufanyia wimbo wako wa mwisho wa 'Abiro iei Nyasaye' ulikuwa wimbo wa utabiri na wa kusema kwaheri lala mahala pema peponi ushajaa wako utazdi kuonekana." Aliandika Fibi.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa chama cha ODM Philip kupitia kwa mitandao ya kijamii alituma rambirambi zake na kusema,

"RIP DR. DOREEN AND LADY MAUREEN. YOU WERE GREAT LADIES.IN YOUR DIFFERENT CAPACITIES; YOU HAVE LEFT A MARK.FARE-THEE-WELL OUR DEAR SISTERS."

Hizi hapa baadhi za risala za rambi rambi kutoka kwa wakenya na marafiki;

Leodawo Leodawo May her soul rest in peace, my sincerest condolences to the family and friends.

Koth Lili you suffered a lot in pain and now you have fought the last fight all in all the up man is to judge, Rip

Bornface Otieno Nyawawa Soooo sad may our beloved artist nyaseme Rip

Shekameta Okembia My heart felt condolences to the family.May her soul rip 😭. We love you but God love you most.😭

Aduda Safan Siguna What’s happening to Ohangla musicians nowadays? May God rest her soul in peace.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.