Tazama picha za mwanamke aliyeanguka Thompson Falls akichukua picha

Familia moja ya Kenya inaomboleza kifo cha binti yao aliyeteleza na kaunguka katika mto kwenye  Thompson falls huko  Nyahururu.

Jemimah Oresha  alikuwa amewatemebela jamaa zake  alipomtaka  kakake kumpeleka katika eneo hilo maarufu .

Kakake alikubali  na jumapili wawili hao walianza safari ya kwenda thoson falls  amako Jemimh aliona jiwe ambalo aliamua alitaka appigwe picha akiwa amesimama juu ya jiwe hiolo katikati ya mto .

Akipiga pozi ili picha zichukuliwe aliteleeza kwa bahati mbaya na kuanguka mtoni  huku kakake akiangalia bila kuweza kumuokoa dadake .

Kulingana na Mangafu dadake  alifaa kusafiri kwenda nyumbani kwao Kitale siku ya jumatatu  lakini  hilo halitafanyika kwani hadi sasa mwili wake haujapatikana .

Nyahururu Falls   ni maporomo ya maji yeye urefu wa  (243 ft)  katika mto  Ewaso Ng’iro  katikati mwa Kenya  na kilomita kadhaa kutoka  ziwa  Ol Bolossat