Tazama picha za mwanawe mwanahabari wa runinga ya Citizen Stephen Letoo

Kitengo cha uzazi ni jambo ambalo kila wanandoa hungoja kwa hamu ilhali si wote upata bahati ya kuwa wazazi licha ya wao kuoana, lakini kwa mwanahabari Stephen Letoo uzazi ni zawadi ambayo hatowahi sahau maishani mwake.

Kulingana na Letoo,

"BABIES ARE LIKE LITTLE SUNS THAT, IN A MAGICAL WAY, BRING WARMTH, HAPPINESS AND LIGHT INTO OUR LIVES..A BABY IS GOD’S OPINION THAT LIFE SHOULD GO ON..THEY ARE THE BRIDGE TO HEAVEN..

GOD DROPPED US BABY SANTINO L’EYIAN L’ETOO @SANTINOLEYIAN AS A SPECIAL GIFT, I GIVE HIM TO THE WORLD, AS A SIGN OF PEACE❤." Aliandika Letoo.

Santino alifikisha mwaka mmoja siku chache zilizopita, mbali na ukakamavu wake kama mtoto ana sura ya kupendeza na urembo wa kipekee, huku akimsherehekea mwanawe Letoo alikuwa na ujumbe huu wa kumnakilia mwanawe.

"Umetimiza mwaka mmoja hii leo? Wow muda umeenda kwa kasi mno wewe ni mtoto ambaye kila mzazi angetamani kuwa naye, umekuwa ukitupa zawadi kila siku 

Mwaka mmoja ambao tumekuwa na wewe kwa siku 365, umetupa zawadi kila kuchao, kila siku ambayo umekkuwa nasi mwaka huo mmoja hauwezi badilishwa wala huna malipo

Blow billion candles happy birthday Papito." Aliandika Letoo.

Hizi hapa baadhi ya picha za mwanahabari Letoo na mwanawe;