Tazama picha za video vixen anayetishia kumuondoa Diana Marua

Inaonekana mtoto wa mama Bahati hakutoshelezwa na pesa za muziki wa nyimbo za injili, huku akianza kuimba muziki wa kidunia. Mnamo tarehe 11 Juni, msanii huyo alitoa kibao kinachofahamika kama 'wanani toto si toto.'

Baba huyo wa watoto watatu alianza kuimba nyimbo zake akiwashirikisha wasanii au kikundi cha Gengetone, Boondocks ambao wanafaahamika kwa vibao vyao vya nyimbo za kidunia.

Bahati alikuwa mwerevu zaidi baada ya kutumia picha za kanisa katika video ya muziki wake na Gengetone kuwachanganya mashabiki wake wasione kuwa ameanza kuimba nyimbo za kidunia.

Wimbo ambao Bahati ameutoa unathibitisha kuwa ametoka katika dunia ya nyimbo za injili na kuanza kuimba nyimbo zingine.

Hivi ndivyo Willy Paul alianza kabla ya kuanza kuimba nyimbo za kidunia kabisa na kuingia na miguu yote katika nyimbo za kidunia. Haya basi Bahati ametoa kibao hicho na video vixen mmoja anayetishia kumuondoa Diana.

Mbali na hayo, kibao cha wanani toto si toto ni kibao cha mapenzi na inaonekana mwanamke huyo amechukua moyo wa msanii huyo.

Si vibaya Bahati kuanza kuimba nyimbo za kidunia lakini cha kushangaza ni aliweza vipi kumchukua rafikiye Diana awe Vixen katika kibao chake?

Mashabiki wake walimuonya dhidi ya video vixen huyo, hizi hapa baadhi ya hisia za mashabiki wake;

Aaai baha Diana aliaccept hiyo video 😢😢

 i feel like diana should be the one

the video vixen is Diana’s best friend she’s called 

this is business, ukileta wivu kwa job utakua Mawe? 🤣

Hivi ndo mtu huachwa😂😂

Akyyyyy Diana utanyaganywa bwanako ukionanga tuuuuu na machoooo,,,,,,huyu Dem n🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥