Tokeni hapa ! Akothee afurusha binti zake kwa sababu ya Coronavirus

Msanii  mpenda sakata Akothee amewafukuza wasichana wake wawili dakika chache tu baada ya kuwasili ili kumtembelea .

Mama huyo wa watoto watano  alihamakishwa na hatua ya binti zake kutaka kumpiga hug ilhali walikuwa wamewasili kutoka  uwanja wa ndege. Akothee  aliamua kuwatoa mbio kwa kuwaitia mbwa wake wakali .

Kulingana  naye, Rue Baby na  Fancy Makadia  walikuwa wamewasili na  huenda wana virusi vya Corona  kwani hata hawakuwa wameoga. Katika video alizoweka katika instagram  Akothee ametishia kuwaitia polisi endapo hawataoga  na kujitakasa  na kuziweka nguo zao katika jik  ili kuua virusi

 “They said no hug, stay away from me you idiots, you have just come from the airport and you want to hug me, those airport sits have corona. Go away and shower and get into the swimming pool and disinfect yourselves or else I will call police on you,”  Akothee alifoka .

Rue Baby  anasisitiza  kwamba alikuwa amenawa mikono  lakini mamake hakutaka kusikiza hilo.

  “Corona has no boundaries, it is real, it doesn’t know whether you are my mother or whatever, please don’t bring corona here,”

Alisema

Kwa wiki mbili zilizopita Akothee amekuwa nyumbani   pamoja na mbwa wake akiwaburudisha mashabiki wake kwa video anazoweka mtandaoni .