TRUE LOVE : Jinsi Edwin Abonyo alivyomteka kimapenzi Joyce Laboso .

Miaka 37 iliyopita  maneja  chipukizi katika   kampuni ya mashamba ya chai ya Highlands   huko Kericho  alimwona msichana  mdogo mrembo ambaye wakati huo alikuwa chuoni  . Kumtazama kwa mara ya kwanza kulikuwa hatua moja ya safari  iliyoanza na urafiki kisha hatimaye kumwoa .Edwin Abonyo,  mumewe marehemu gavana wa Bomet Joyce Laboso    alhamisi  alitoa simulizi ya kumbukumbu ya jinsi  yeye na  Joyce walivyokabiliana na vizuizi katika Uhusiano wao  alipojaribu kuishawishi familia ya Joyce kumruhusu kumchumbia binti yao  ili baadaye aweze kumwoa .

Na kama ilivyotajiwa babake  Joyce  Fredrick Laboso  alikuwa mkali sana  na hakutaka kusikia lolote kuhusu uhusiano wa bintiye na Abonyo . Abonyo amesema alipokuwa akitaka kuzungumza  na Joyce Kupitia simu ,binamu yake Sam Ngondi  ndiye aliyekuwa akipiga simu kwanza  kisha Abonyo angeanza kuzungumza tu baada ya kuthibitisha kwamba sauti   katika upande wa pili ilikuwa ya Joyce . Marehemu Laboso atazikwa siku ya jumamosi katika eneo la Koru ,kaunti ya Kisumu .