Trump asitisha msaada wa mabillioni ya dollar kwa Shirika la afya dunia

Wakati ambapo taifa la Amerika na lile la Brazil likiendelea kusajili idadi kubwa ya watu wanaofariki kutokana na virusi hatari vya corona,rais wa Amerika Donlad Trump ameamuru kusitishwa mara moja kwa taifa hilo kuendelea kutoa ufadhili wa mabilioni ya pesa katika shirika la afya duniani WHO

Hatua hiyo huenda ikalemaza sasa mchakato wa WHO wa kupigana bna virusi hivyo hatari ambavyo kufikia sasa vimeathiri uchumi wa taifa mengi ulimwenguni.

Kwa upande wake kiongozi huyo mpwatukaji amesema hatua ya kuondoa ufadhili huo kwa WHO ,umechochewa na hatua ya shirika hilo kukosa kuishinikiza uchina kuelezea chimbuko la virusi hivy hatari.

Mataifa ya Amerika Kusini yapo chini shinikizo kutokana na ongezeko la maambukizi na p[ia idadi kuwa ya watu ambao wanafariki kutokana na virusi hivyo hatari.

Taifa kama la Brazil,chini ya saa 24,watu 1224 wamefariki kutokana na corona huku idadi ya maambukizi ikisalia kuwa juu.

Japo Trump amesema taifa hilo halitaendelea kutoa ufadhili kwa shirika la afya diniani ,amesema pesa hizo zitapelekwa katika mataifa mengine ambayo yanakabiliana na virusi hivyo.

The US would be redirecting WHO funds“to other worldwide and deserving urgent global public health needs.”“The world needs answers from China on the virus. We must have transparency,” Trump amesema.