Tujitayarishe kupiga kura ya BBI, Kinara wa ODM Raila Odinga

Screenshot_from_2019_11_29_10_38_54__1575013168_56727
Screenshot_from_2019_11_29_10_38_54__1575013168_56727
Kinara wa ODM Raila Odinga ametoa taarifa kuwa mapendekezo ya BBI yatapitishwa kupitia kura ya wananchi wala sio bunge la kitaifa.

Raila ameyasema haya katika kongamano la chama hicho hapo jana.

Hii inafuatia tamko la Aden Duale kuwa mapendekezo ya BBI hayana uzito mkubwa na kwa hivyo yanaweza kujadiliwa na kuamuliwa katika bunge.

Mbunge Moses Kuria anahoji kuwa Kenya itagharamika hela nyingi iwapo tutazamia uchaguzi wa kupitisha ama kukana mapendekezo hayo.

Tamko la Raila Odinga huenda likazua msukosuko na maoni kinzani kutoka kwa wabunge wa TangaTanga.

Raila aliwasifia wabunge wa ODM kwa kusimama kidete katika kuhakikisha 'Handshake' kati yake na Uhuru imedumishwa.

"Hii ripoti ni ya Wakenya na haitapelekwa bunge. Wakenya wataamua wenyewe kuihusu," Raila alisema.

Mwandani wa Rais Uhuru Maina Kamanda alikuwa katika kikao hicho cha kufungua ofisi mpya za chama hiki.

Tamko la Raila liliungwa mkono naGladys Wanga, Hassan Joho,  na John Mbadi miongoni mwa vingozi wengine.

"Mimi ni mbunge lakini nasema bunge haliwezi kuachiwa ripoti hii. Ni lazima iende kwa wananchi," Mbadi

Joho alipuuzilia mbali swala la bunge kujadili na kupitisha BBI,

"Wanaota, hao hawakuanzisha safari hii. Wajipange, kama ni kuonana tutaonana mashinani kwa wananchi,"

Inahofiwa kuwa siasa za BBI zinaweza kupandisha joto la kisiasa nchini.