Tuju Aitisha mkutano wa MCA’s wa Jubilee kabla ya uchaguzi wa spika kesho

Chama cha Jubilee kimeitisha mkutano wa waakilishi wake wa kaunti 66 kwa mkutano wa dharura leo utakaofanyika makao makuu ya cjhama hicho ,pangani .

Mkutano huo unafanyika siku moja kabla ya waakilishi wa kaunti ya jiji kufanya uchaguzi wa kumteua spika mpya baada ya Beatrice Elachi kujizulu siku ya jumanne .

Katika barua kwa kiranja wa wengi katika bunge hilo ,katibu mkuu Raphael Tuju amemtaka  Paul Kados kuhakikisha kwamba viongozi wote wa chama hicho wanahudhuria mkutano wa leo .

Wakati huo huo  waakilishi wanane wa Jubilee  watafika mbele ya kamati ya nidhamu inayoongozwa na  Tuju kabla ya mkutano wa leo kuanza . siku ya Jumanne  mwenyekiti wa kitaifa wa Jubilee Nelson Dzuya, na waakilishi hao walitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ya nidhamu saa nne asubuhi .

Waliotakiwa kufika mbele ya kamati hiyo ni  pamoja na ;John Kamangu Nyumu (Ruai), Millicent Mugambi (Ziwani) Jeremiah Karani (Kayole Central Ward) na Charles Thuo (Dandora Three MCA) wengine ni  June Ndegwa, Joyce Kamau, Susan Makungu na  Margaret Mbote.