Tukio la Akothee kuanguka ghafla na kuzirai stejini , ni kiki au ni ukweli?

jmdi2qhmdqhqx7v15de4b38974924
jmdi2qhmdqhqx7v15de4b38974924

Tukio la Akothee kuanguka ghafla na kuzirai akiwa stejini limewafanya wengi kuzungumza sana katika mitandao ya kijamii.

Tukio hilo limewashtua watoto wake huku binti zake wakimtumia jumbe za kumtakia afya njema.

Kifungua mimba Vesha Okello, ambaye alishtuka sana baada ya kupokea habari mbaya za mamake kuzirai akitumbuiza aliandika ujumbe wa kumpa pole.

Tazama kipande hiki cha video:

https://www.instagram.com/p/B5hzFTzFV2s/

Wengi wa mashabiki walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa burudani wikendi katika fiesta waliposhuhudia kisa hiki.

Wengi walimtumia jumbe za kusema pole na kumtakia afueni ya haraka.

Ila kuna shabiki na ambaye aliuliza iwapo kweli ni ukweli au ni kiki?

Katika juhudi za kuvuma na kuzungumziwa katika blogu na magazeti kuu nchini, mastaa wa nyimbo wanaweza fanya chochote ilmuradi tu kusukuma mauzo ya bidhaa fulani au ata sanaa yao kuvika levo za juu zaidi.

Mwende_moh aliuliza,

Kivipi? Kwani wapiga densi wake walijua ataanguka?

Maoni kinzani yanatolewa kuhusiana na kisa hiki.

Hivi unadhani kwamba Akothee anafanya kiki?