'Tunamfuata Raila kama Ng'ombe kwa sababu tunahofia kupoteza nafasi zetu', Junet amwambia Duale

EbMsBgsWAAAeNLF.jfif
EbMsBgsWAAAeNLF.jfif
Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed aliibua kicheko bungeni baaada ya kudai kuwa huwa wanamfuata Raila Odinga kama Ng'ombe ili kuepuka kupoteza nyadhifa zao katika kamati mbalimbali bungeni.

Junet alisema hayo kwa kumshauri Aden Duale ambaye alitimuliwa kama kiongozi wa wengi bungeni baada ya wabunge wa chama cha Jubilee kupitisha hoja ya kutokuwa na imani na utendakazi wake.

Junet alisema kuwa siasa za siku hizi ni tofauti zikilinganishwa na za zamani kwani ukienda kinyume na kiongozi wako wa chama unajikuta katika njia panda.

Amesema amejifunza mengi baada ya kuona Duale akitimuliwa na hivyo ataendelea kuwa mwaminifu kwa baba na hata kumshabikia kila uchao.

"To the former majority leader, my brother when you see us following baba like cows, we are fearing consequences like the ones you facing now. "It is a good experience for me, I will be more loyal than I was and I will sing baba through out," alisema Junet

Aliongezea kuwa wabunge wako tayari kumsaidia kiongozi wa wengi kwa sasa Amos Kimunya ili kufanikisha utendakazi wake.

"When the going gets tough, do not die. Do not say 'I'd rather die than resign' just stay alive because we shall support you," Mohammed

Duale ambaye ni mbunge wa Garissa mjini aliondolewa kama kiongozi wa wengi tarehe 22 Juni mwaka huu wakati wa mkutano wa wabunge wa Jubilee uliochukua dakika 22.