Tupo tayari sasa. Farasi wa ODM atangazwa kusubiria mtifuano Kibra.

unnamed__4___1567928306_95012
unnamed__4___1567928306_95012
Ni bayana kwamba sasa Benard Okoth kakake marehemu Ken Okoth atamenyana na farasi wa Jubilee Macdonald Mariga, Eliud Owalo wa ANC na Khamisi Butichi wa chama cha Ford-Kenya katika mchuano wa kumtafuta atakayekua mbunge wa Kibra.

Okoth, almaarufu kama Imran aliwabwaga wagombeaji 9 chini katika zoezi tulivu lililofanyika jana jumamosi. Okoth alitangulia kwa kura 4,382.

Waliomfuta hatua chache nyuma ni Peter Orero (1,218), John Milla Otieno (906), Ben Musungu (524), Christone Odhiambo (417), Tony Ogola (381), Stephen Okello (228), Brian Owino (127), Reuben Ojijo (52) na mwisho Eric Obayi (45).

Soma hadithi nyingine:

Okoth sasa ana jukumu kubwa la kuwarai wakaazi wa Kibra wampe nafasi ya kuendeleza juhudi za kakake. Tarehe 7 Novemba ndio itakuwa siku ya kutofautisha farasi na punda katika mtifuano wa kumrithi Ken Okoth.

Macho yote sasa yanatazama kuona Jubilee ikipenya ngome ya Raila Odinga. William Ruto alitembelea eneo bunge hilo na kuahidi kuwa atarejea na kikosi chake kizima kumpigia debe MacDonald Mariga.

Soma hadithi nyingine:

Ubuyu mtaani ulitamba kuwa huenda Mariga alikuwa farasi aliyepenyezwa na William Ruto. Aidha mariga alikana taarifa hizi na kusema kuwa hatumiwi na mwanasiasa. Chama cha ODM kilikuwa kimetangaza awali kuwa zoezi hilo litakuwa la wazi.