Twaomba uwe mshindi! Wakenya wazidi kumuombea Ken Okoth

Wakenya kutoka tabaka mbali mbali katika mtandao wa kijamii wa Twitter wanazidi kumuombea mbunge wa Kibra, mheshimiwa Ken Okoth.

Hii ni baada ya picha yake Ken Okoth ambaye amekuwa akipokea matibabu ya ugonjwa wa saratani, nchini Ufaransa, kuchapishwa mtandaoni na balozi wa Kenya nchini Ufransa, Judi Wakhungu hapo jana baada ya mkutano kati ya wawili hao.

Katika ujumbe wake, Wakhungu alisema kuwa katika maongezi yao, Okoth aliwapa muktasari kuhusu miradi yake ya masomo na mipango aliyo nayo ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo imefikia wanafunzi wengi.

Soma habari yake hapa,

Courtesy call from Hon. Ken Okoth (Kibra). He updated us on many issues including his impressive education projects & his plans for increasing them to reach many students. He is also keen to use Sports Diplomacy to expand his students’ horizons.

 

Pindi tu picha hizo zilipo chapishwa wakenya wenye huruma walimpa moyo mheshimiwa huku wakiomba kuwa awe mshindi katika vita anavyokumbana navyo.

Haya ni baadhi ya ujumbe alizopokea.

Bishopwild: Ken Mr. You will be well Sir. God has a plan for YOU.. Good work as always.. Be well.

OneJacobKelly: Brother Ken Okoth ~ We are with you in Prayers. You shall overcome.

James Jakabido: The resilience and the way this man has accepted his condition is so sweet,some could be in deep denial by now Honourable am so honored with your determination and courage to serve your people

Ernest: I appreciate the fact that Hon.Ken Okoth shared his mind with prof Judi Wakhungu. .what a clear impression of brotherhood . @ Ken Okoth, you will be well in Gods' favour

Aggy Wamukoya: May God's healing be upon you mheshimiwa!