uefa

Ubashiri wa ligi ya mabingwa ulaya

Raundi ya tatu ya ligi ya mabingwa ulaya utakuwa unasakatwa leo usiku huku klabu mbalimbali zikitarajia kuandikisha ushindi.

Juventus vs Lokomotiv Moscow

Klabu ya Juventus ambalo kwa sasa linaongoza katika kundi D na pointi 4 watakuwa wanamkaribisha Lokomotiv Moscow nyumbani kwao Allianz.

Maurizio Sarri ambaye ni mkufunzi wa Juventus ana matuimaini kuwa wachezaji wake watashinda mechi hilo hii ni baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Atletico Madrid katika raundi ya pili.

Lokomotiv Moscow katika raundi ya pili waliwanyuka klabu ya Bayer mabao mawili kwa moja hivo basi wanatarajiwa kuleta ushindani mkubwa. Utabiri wangu ni Juventus watashinda kwa mabao 3-1.

juve

Galatasary vs Real Madrid

Ni mchuano ambao umesubiriwa kwa hamu kwani mashabiki wa Real Madrid wanatarajia kupata ushindi baada ya kuadhibiwa vikali na klabu ya PSG mabao tatu kwa bila, na katika raundi ya pili kutoka sare ya mabao mawili na Club Brugge.

Kampuni bora 100 za kufanyia kazi

 Galatasary kwa upande wao wanatarajia angalau kujinyakulia pointi tatu kwani kwa sasa klabu hizo mbili zina pointi moja. Utabiri wangu ni klabu hizo mbili zitatoka sare tasa ya mabao mawili.

ramos

Tottenham vs Crvena Zvezda

Mauricio Pochettino ambaye ni mkufunzi wa klabu ya Tottenham ana matumaini kuwa vijana wake wataandikisha ushindi usiku wa leo. Tottenham bado hawajapata ushindi tangu msimu huu wa ligi ya mabingwa ulaya uanze.

Klabu ya Crvena kwa upande wao wanatarajia kupata ushindi uwanjani White Hart Lane. Kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili katika kundi B wakiwa na pointi 3. Utabiri wangu ni Tottenham watashinda mchuano huo kwa mabao 3-2.

tote

Kinaya siku ya Mashujaa, wakenya wafunguka

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments