Oh No!Tazama Video Inavyoonyesha ukatili wa Jamaa akimpiga mfanyikazi wake

ukatili
ukatili
Maajuzi tu wakenya wamejionea video ya   raia mmoja wa Uchina akimcharaza viboko mkenya kwa kuchelewa kuja kazini katika mkahawa mmoja kileleshwa .Lakini kuna video nyingine inayosambazwa katika mitandao ya kijamii inayonyesha  jamaa akiwa amefungwa kwenye kiti na kutandikwa vibaya sana na mtu anayeonekana kuwa mwajiri wake . Haijajulikana video hiyo ilichukuliwa wapi au wahusika ni akina nani lakini inamwonyesha mtu mwenye asili ya  ki ashia akimtandika kwa ukatili jamaa mmoja kutumia ktu kama kibomba kigumu cha  mpira .

https://twitter.com/YusufJumaKenya/status/1229740620551462912

Mwathiriwa  analia kwa uchungu lakini  maskini yule katili hamuachi. Wakenya wametamaushwa na video hiyo huku wengine wakidokeza kwamba mateso kama haya ndio wanayopitia wakenya wengi wanaotoka Kenya kwenda mashariki ya kati kutafuta kazi .Ingawa mwathiriwa katika video hii hajatambuliwa ,ukatili huu ni wa kushangaza na huenda kuna wengi wanaopitia mateso kama hayo .