Uhuru 2

Uhuru afanya mabadiliko katika serikali

Rais Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika wizara za serikali kwa lengo la kuboresha utoaji huduma.

Uhuru 2
Katika agizo la rais siku ya Ijumaa, Uhuru aliunganisha idara ya usalama wa ndani na ile ya uhamiaji.
Idara ya kitaifa ya mambo ya ndani na ile ya huduma kwa wananchi sasa zote zitakuwa chini ya wizara mambo ya ndani na uratibu wa serikali ya kitaifa.

 
Idara ya kunyunyizia mashamba sasa imewekwa chini ya wizara ya maji kutoka wizara ya kilimo
Wizara hiyo sasa itajulikana kama wizara ya maji,usafi na unyunyiziaji. Wizara ya kilimo pia imebadilishwa jina na sasa itajulikana kama wizara ya Kilimo,mifugo na uvuvi.

 
Kitengo cha rais cha kuimarisha huduma kwa wananchi (The President’s Delivery Unit) kimehamishiwa katika wizara ya mambo ya ndani.

 

 

Mabadiliko haya yanaanza kutekelezwa mara moja.

Photo Credits: File

Read More:

Comments

comments