Majuto ni Mjukuu:Uhuru amemsaliti Ruto –Wazee wa jamii za kikuyu na Kalenjin wadai

uhuruto
uhuruto
Kundi la wazee kutoka jamii za wakalenjin na wakikuyu  kutoka rift valley sasa linasema kuwa rais Uhuru Kenyatta anamhujumu naibu wake William Ruto kutumia  asasi za  serikali

Wazee hao wamezungumza huku washirika wa Ruto wakianza kupeleka makabiliano dhidi ya rais Kenyatta katika ngome yake  na kubadilisha mageuzi katika  takriban kaunti mbili yaliodhinishwa na rais .  Malumbano ambayo yamekuwa  yakitokota katika  chama cha Jubilee huenda yakalipuka wakati wowote  huku pakiibuka ripoti kwamba rais Uhuru Kenyatta anapanga kufanya mageuzi ya kunadhifisha serikali yake kwa kuwaondoa baadhi ya washirika wa Ruto katika nafasi za uongozi chamani na bungeni .

Wakizungumza na gazeti la  kiongozi wa baraza la wazee wa kikuyu Rift valley  Gilbert Kabage a na  mwenyekiti wa baraza la wazee  wa kalenjin Myoot  askofu mstaafu   Paul Leleito  wamedai kwamba Uhuru anamfadhaisha Ruto kupitia washirika wake . Wamedai kwamba kimya cha rais Kenyatta huku naibu wake akipigwa vita ni dhihirisho tosha kwamba ameidhinisha mashambulizi hayo .Kabage  amemtaka rais Uhuru kujitokeza wazi na  na kutangaza iwapo atatekeleza makubaliano yao ya mwaka wa 2013 kwamba tamuunga mkono naibu wake kuchukua usukani mwaka wa 2022 badala ya kumhujumu .

“   Kile  ambacho Uhuru anamfanyia Ruto ni vitendo vya  kale ambavyo havina ustaarabu . tumeshuhudiwa machafuko ya kikabila  1992,1997 na mwaka wa 2007-2008 . Tunataka kuwamabia wahusika kwamba hatutakubali kurejeshwa katyika mondo huo tena’ amesema

Wakosoaji wa Naibu wa rais wamekuwa akidai kwamba washirika wake wanatumia vitisho vya ghasia  Rift valley ili kuwalazimisha  watu wa jamii ya kikuyu kumpigia kura mwaka wa 2022.

“ Iwapo Uhuru anataka kufanya muungano na Raila basi afanye hivyo bila kumfadhaisha Ruto na sarakasi hizi zote . wakenya wataamua kiongozi wao wakati utakapofik’ Kabage amesema

Amesema iwapo Ruto hangemfanyia kampeini rais Kenyatta kwa nguvu zake zote  basi Uhuru hangekuwa  rais .

“Uhuru  anafaa kukumbuka vizuri ‘handshake’ aliofanya na Ruto katika uwanja wa Afraha ,nakuru  na ahadi aliotoa . aAlitoa ahadi hiyo  mbele ya ummati wa watu na tutaendelea kutii ahadi hiyo’ amesema

Lakini akimjibu mwenyekiti wa baraza la jamii ya wazee wa jamii ya kikuyu Wachira Kiago amesema kauli hiyo ya Kabage ni  hatari na isiyo na uajibikaji.

“Uhuru  kila mara anazungumzia kuhusu kuwaunganisha wakenya . sasa inakuwa vipi kuna wanaosema kwamba hilo ni kuzigonganisha jamii mbili?’ alihoji

“ Ni jambo la kusikitisha kwamba matamshi kama hayo yametoka kwa wazee . kuna masuala mengine ambayo taifa linakabiliana nayo kwa sasa na wazee wanafaa kuyangazi’ aliongeza .

Naibu wa rais mwenyewe amedai kwamba huenda asasi za utawala na serikali zimegeuzwa kuwa silaha ili kumpiga vita . Amekuwa akikosa kuonekana katika makabiliano ya serikali dhidi ya  janga na virusi vya Corona  ambavyo vimeathiri uchumi wa taifa. Hivi karibuni hata hivyo Ruto amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kunukuu aya za biblia  ili kutuma jumbe fiche kueleza makabiliano dhidi yake na  kutoa taswira ya kilicho fikrani mwake .