Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambi rambi kuifariji familia ya Henry Masaku Ngei aliyefariki kwa sababu ya saratani ya korodani siku ya jumatano usisku
Ngei, mwenye umri wa miaka 74, ni mwanawe wa kwanza wa mpiganiaji wa uhuru na mbunge wa zamani wa kangundo Paul Joseph Ngei
Katika ujumbe wake kwa familia ya Ngei Uhuru alimtaja mwendazake kama mfantyibiashara na mzalendo ambaye alifanya kazi kwa bidii kulistawisha taifa .
" kifo chake kimeinyim akenya mtu ambaye biashara zake katika sekta ya utalii na kilimo iliwapa maelfu ya wakenya nafasi za kazi’ Uhuru amesema
" katika maisha yake yote Ngei alichangia umoja wa mafanikio ya nchi na ushauri wke wenye busara utakosekana’
Hadi kifo chake Ngei alikuwa akiendsha hoteli ya Tala Motel katika mji wa Tala na alikuwa mkulima katika eneo la Kangundo ,Machakos .