Uhuru atoa sababu za kuagiza mabadiliko ndani ya ViuSasa na Skiza

viu sasa
viu sasa
Rais Uhuru Kenyatta ameelekeza mabadiliko kwa muundo wa ukusanyaji kwa watoa huduma - Skiza na Viusasa.

Uhuru alisema kuwa ni uamuzi wake kuona kuwa washika dau wote waliosajiliwa wanapokea malipo yao.

"Skiza and Viusasa will be eliminated because they sit outside the collection management organisations," Alisema.
Rais Kenyatta alizungumza siku ya Jumanne wakti alipohutubia taifa kutoka ikulu ya rais, mjini Mombasa.
"I direct the Interior Ministry to ensure PSV, hotels, broadcasters, meet all their obligations in paying tariffs. This will be for renewing licences," Alisema.

Uhuru alisema malipo yote ya wanaozalisha vipindi humu nchini sasa yataelekezwa kupitia Kenya Copyright Board.

Alisema kuwa wazalishaji vipindi sasa watatumia majukwaa hayo  moja kwa moja.

"Kenyans are talented and music industry lucrative. They are getting low returns and we must allow their investments to pay off. I believe that in this way we can do exceptionally well. I direct the ICT ministry to work with stakeholders to resolve the legacy issues that have plagued the rights issue," he said.