Uhuru azungumzia BBI, afutilia mbali tetezi za kusalia serikalini

Uhuru-compressed
Uhuru-compressed
Rais Uhuru Kenyatta amefutilia mbali tetezi kwamba yeye ananuia  kusalia  serikalini hata  baada ya kipindi chake cha  miaka mitano  kuisha 2022.

Wito wa maridhiano BBI umekuwa ukisemwa kwamba unanuia kuongeza nyadhifa za uongozi kwa Uhuru na Raila Odinga.

"Mimi sitaki kazi mimi nimechoka. BBI ni kuhakikisha ya kuwa hakuna mKenya atamwaga damu katika nchi yetu," alisema.

 Uhuru alisema hayo alipoizindua rasmi Nairobi Expressway Jumatano.
Uzinduzi huo ulifanywa katika Cabanas Mombasa Road.

"Na  hiyo bara bara tutafikisha pamoja na viongozi wengine.. msidanganywe jameni.. penda nchi yenu..mjipende nyinyi wenyewe..sina shaka ati tutaboa hii safari," Uhuru added.

Uhuru amesema kwamba  lazima Wakenya waungane ili nchi hii iendelee.

"Tusaidiane lakini tusimwage damu. Tushirikiane kwa sababu heshima sio utumwa," amesema.

Naye naibu wa rais William Ruto amesema kwamba BBI haitadumu bali itaangushwa. Akifanana na mswada wa  Punguza Mzigo, Ruto alisema kwamba BBI haitapokolewa na wananchi.

Ruto amesema kwamba hatima ya taifa hili haitaamuliwa na watu wawili wanaokaa kwenye hoteli na kupanga maazimio hayo.

Awali, Ruto alikuwa ameahidi kupinga ripoti ya BBI ambayo inanuia kuongeza nyadhifa za uongozi za baraza la kitaifa.