Uhuru hatamkubalia mwizi kukalia kiti cha urais - Murathe

Murathe.1
Murathe.1
Rais Uhuru Kenyatta hatamkabidhi mwizi mamlaka, kulingana na aliyekuwa naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe.

Murathe aliwambia waumini siku ya Jumapili kuwa Uhuru ameapa kwamba hataruhusu mwizi kutawala Kenya.

"I know one thing for a fact that: Uhuru will not leave the country to thieves and a thief will not rule after him because Uhuru is not a thief," Alisema katika kanisa la PCEA Ngewa eneo la Githunguri, Kiambu.

Murathe alisema Naibu Rais William Ruto na wafuasi wa Tangatanga wameacha kuwatumikia wakenya na sasa wameanza kutoa ahadi vile watafanya kazi mwaka 2023 na ilhali kuna miaka mitatu kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

"You were given by Kenyans five years and another five years to work for them. Jubilee leaders are in government, but they have stopped doing development and are now telling us what they will do in 2023. Tell me – if you are in your right senses – can you be given work by Kenyans in 2017 and two years down the line you tell them no let's stop now we will deliver in 2022 once you make me President?" Murathe alisema akichangisha pesa za kujenga makao ya wazee.

Murathe aliwashtumu viongozi wa Jubilee kutoka eneo la Mlima Kenya kwa kutumiwa kumpiga vita rais Kenyatta. Alisema baadhi ya viongozi wamekuwa hata wakimtusi rais.

Mbunge huyo wa zamani wa Gatanga amewataka wanasiasa wa Mt Kenya kujifunza kutoka kwa wenzao wa Rift Valley.

"Other leaders asked development projects and have assured Uhuru strong support when he was in Eldoret. But back home, they (Mt Kenya leaders) are focused on the 2022 narrative.

"We as voters in this region are wondering what they want to do in 2022 that they can't do now. We still have three years before the next polls and it seems they have forgotten Jubilee is the government. The President listens to his people. In fact, Uhuru has outlined what Kenyans want him to do and we all know."

Aliwataka wafuasi wa Tangatanga kuachana na katibu mkuu wa Jubilee Raphael Tuju. Alisema Tuju aliteuliwa na rais na katiba ya chama hicho inasema kwamba atahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa chama hicho.

Alisema mtu aliyesaidia sana kumaliza machafuko ya kisiasa ya mwaka 2007 ni aliyekuwa Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka alipokubali kufanya kazi na rais Mustaafu Mwai Kibaki. Alisema Kalonzo hakuanza kufanya kampeni ili awe rais au kuunda kundi la wabunge kupinga sera za kibaki.

Murathe alimkashifi naibu rais William Ruto kwa kutoonyesha nia ya kukabiliana na ufisadi.