Uhuru kujaza nafasi ya waziri Henry Rotich

NA OLIVER MATHENGE

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kumtaja kaimu waziri wa fedha baadaye hivi leo (Jumatatu)

Rais pia anatarajiwa kumteua kaimu katibu wa kudumu katika wizara ya fedha kuambatana na tangazao lake wakati wa hotuba yake bungeni mwezi Aprili.

Akihutubia wabunge, Uhuru alisema kwamba afisa wa serikali ataacha kushikilia wadhifa wake punde tu anaposhtakiwa Mahakamani.

Habari zaidi:

Inatarajiwa kwamba rais atataja kaimu waziri kutoka mawaziri wake wa sasa wanaohudumu, kwa sababu ikiwa atataja mtu wa nje basi atahitaji kuidhinishwa na bunge kabla ya kuapishwa.

Duru katika afisi ya rais ziliambia gazeti la The Star kwamba Uhuru atafanya tangazo hilo punde tu Roticha atafikishwa mahakamani.

Hii inafuataia tangazo la mkurugenzi mkuu wa mshtaka Noordin Haji akiagiza kukamatwa kwa Rotich na Thugge.

"Hapatakuwepo na pengo katika ofisi hii. Ni taasisi muhimu ambayo inaweza kulemaza shughuli za serikali," duru katika ofisi ya rais zilieleza.

Uhuru alikuwa tayari ameelezewa kuhusiana na njama za kumkamata Rotich na mapema Jumatatu alikuwa akishauriana na wanaohusika kuhakikisha shughuli za kawaidi zinaendelea.

JE ROTICH NI NANI?

Rotich aliteuliwa waziri wa fedha Mei 2013 katika baraza la mawaziri la kwanza la rais Uhuru Kenyatta. Katika kipindi cha miaka sita iliyopita, Rotich amekuwa na jukumu la kusimamia hazina ya kitaifa, ikiwemo kuongoza mikakati ya matumizi bora ya fedha za umma.

Kabla ya kuteuliwa waziri, Roticha alikuwa mkuu wa kitengo cha uchumi wa sekta kuu nchini (Macroeconomics) katika wizara ya fedha, tangia mwaka 2006. Kabla ya kujiunga na wizara ya fedha, Roticha alifanyakazi katika idara ya utafiti ya Benki Kuu nchini tangu mwaka 1994.

Kati ya mwaka 2001-2004, alikuwa katika shirika la fedha duniani IMF, ofisi ya Nairobi akifanya kazi kama mwana uchumi.

Rotich ana shahada ya uzamili (masters) katika masuala ya usimamizi wa umma kutoka taasisi ya Harvard Kennedy, Chuo kikuu cha Havard, Marekani. Pia anashahada ya uzamili katika maswala ya uchumi na shahada ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, nchini Kenya.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO