Ujumbe wa kumdhalilisha Gavana kwenye Facebook yamtia Taabani Mwanaume

Bomet Man
Bomet Man
Mwanaume  anayetuhumiwa kwa kutuma ujumbe wa kumdhalilisha gavana wa Bomet Hillary Barchok katika mtandao  wa Facebook alishtakiwa  Jumanne .

Dominic Kiplangat mwenye  umri wa miaka 31 alishtakiwa kwa makosa mawili ya kuchapisha ujumbe wa kudhalilisha na dharau kwa mamalaka ya afisa ya umma kwenye vyombo vya kielektroniki .

Kesi hiyo iliskizwa kortini  Septemba 22 na Oktoba 14 katika eneo la Bomet Kati.

Ujumbe huo ulisema hivi :

"Je bosi wako anajua kwamba yeye ni "Kabana" kutokana na kifo na cheti cha kifo cha mama wetu mpendwa?" Hivi sasa analipia tendo la ndo la mara moja kwa kima cha shilingi  milioni 2 bila uchungu wowote."

Kifungu cha kesi yake kinaonesha kwamba ujumbe huo wa kudhalilisha afisa ya gavana  Barchok ulisambazwa mtandaoni.

Mshukiwa huyo alitiwa mabaroni Jumatatu na wajasusi kutoka kituo cha Bomet.

Akiwa kortini, hakimu mkaazi wa mahakama ya Bomet Kipkirui Kibelion alisema kwamba mshukiwa alikana mashtaka hayo.

Wakili wa mshukiw a alimsihi jaji ampe adhabu ya dhamana isiyo ya juu sana kwa kuwa mteja wake ni yatima na kitinda mimba anayetegemewa na nduguze.

"Mteja wangu anakaa karibu na kortini, hawezi akatoroka na tunakuomba umpe dhamana au bondi atakayoweza kulipa" Kipngetich alisema.

Jaji kibelion alimwachilia kwa dhamana ya shilingi 30,000.

Kesi hiyo itaskizwa Oktoba 31.