Ujumbe wa mamake Hamisa Mobetto baada ya tuzo la gari

Ama kwa hakika,Hamisa hakutudanganya aliposema kuwa maisha upande wake ni matamu kwani binti huyu anaendelea vyema kweli maishani.

Kidosho Hamisa ameonekana kama baraka kwa mama yake mzazi kwa kutumia pesa zake anazozipata kupitia usanii wake na biashara zake, ameweza kumbariki mama yake na gari nzuri kweli.

Kama desturi ya wazazi,endapo mtoto amefaulu maishani wazazi au waliomlea mtoto huyu watajawa na furaha si kidogo kwani kupitia kufaulu huku, ni wazi kuwa mtoto huyu alitilia maanani yte aliyofunzwa akiwa mchanga na kusadiki methali,asiyeskia la mkuu huvunjika guu.

Aidha ni wazi kuwa mtoto huyu anajifunga kibwebwe kufaulu maishani na si kulaza damu tu.

Hebu tazama vile ambavyo mama yake Hamisa alifurahia.