Uliwacha mrembo wetu Tanasha kumkibilia Hamisa?,huna haya kweli

NA NICKSON TOSI

Diamond kwa mara ya kwanza amezungumzia uvumi kuhusiana na  kuwachana kwake na Tanasha majumaa kadhaa baada ya uvumi huo kuenea katika mitandao ya kijamii.

Katika ukurasa wake wa Instagrama alipokuwa anazungumza na mashabiki wake, Diamond aliulizwa swali na shabiki wake wa karibu afafanue ni kwanini wamekuwa kwa muda mrefu hawaonekani pamoja na kidosho huyo kutokea Kenya.

Kama njia ya kukwepa swali hilo, Diamond alimjibu shabiki huyo akidai kuwa hilo ni swali la kibinafsi ambalo hawezi kulijibu kwa mitandao ya kijamii.

Tanasha yuko wapi, aliuliza shabiki.

Diamond kama njia ya kuficha ukweli alionekana mchangamfu alipokuwa anajianda kujibu swali hilo na kudai kuwa.

"Ni swali ambalo linahusiana na familia yangu na ambalo singependa kulijibu kupitia mitandao" alisema Diamond.

Jibu hilo fupi kutoka kwa Diamond lilikuwa dhihirisho kuwa alikuwa anazima maswali yaliyokuwa yanataka azungumzie maswala ya uhusiano wake na Tanasha ambayo ulisambaratika majumaa kadhaa yaliyopita.

Wiki chache zilizopita Tanasha alitoa jina la Diamond katika majina ya mtoto wake, dhihirisho tosha kuwa mambo hayakuwa mazuri baina ya wapenzi hao wawili.

Mamake Diamond pia alitoa picha zote alizokuwa amepiga na Tanasha wakati mapenzi baina ya mwanawe na Tanasha yalikuwa yamenoga .

Mzozo baina ya Diamond na Tanasha uliibuka pale alipokosa kuhudhuria uzinduzi wa albamu ya Tanasha aliyokuwa anaifanya Nairobi mapema mwezi jana mwaka huu.

Katika uzinduzi huo Diamond aliripotiwa kurejea Tanzania kwa kile kilisemekana kuwa ni kushughulikia shughuli ya dharura iliyokuwa imetokea.