UNGAMWE: Wanawake Mtaa Wa Kikuyu Wanaitisha Pakiti Ya Unga Ili Waanike Nanga

liondeh5
liondeh5
Kila siku katika kipindi nambari moja nchini cha Mbusii na Lion Teketeke kuna kitengo maarufu cha 'Ungamwe Vindialala' ambacho huja mida ya saa kumi kila jioni.

Kitengo hicho huwapa waskilizaji fursa ya kupigia watangazaji, Mbusii na Liondeh simu moja kwa moja na kuangazia tabia na masaibu yanayotokea mitaani. Nia kuu ya kitengo cha Ungamwe Vindialala ni kuanika tabia ambazo haziambatani na sheria au maadili kamili.

Siku ya Jumatano, mskilizaji mmoja kutoka mtaa wa Kikuyu kaunti ya Kiambu aliwashangaza watangazaji hao wawili pamoja na mamilioni ya waskilizaji, aliposimulia jinsi wanawake wa kutoka eneo hilo wanavyotumia chakula kufanya ukahaba.

Kulingana na jamaa huyo kwa jina la utani 'Gos' wanawake hao wana tabia ya kuomba kilo moja ya unga wa ugali kama malipo yake ili ashiriki mapenzi nao almaarufu 'Kuanika nanga'.

"Mbusii unajua nini, hawa wamama huku Kikuyu wana wana sana." Alianza kusimulia 'Ghos'. "Unakutana na mama saa moja ya jioni anakuambia niaje ninunulie ka unga kilo moja halafu nikuanikie." Alindeleza usimulizi wake bwana Ghos.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be