Unyama ulioje? Mwanamme amuua mkewe kwa kumkata kichwa Isiolo

Wakaazi wa  Kangutu huko Isiolo wametamaushwa na kisa cha  mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 28 kumkata kichwa mkewe  kutumia panga baada ya ugomvi wa kinyumbani .

Baada ya tukio hilo David Kiringori alijisalimisha katika kituo kidogo cha polisi cha  Kulamawe akiwa amembeba mtoto wao wa umri wa miaka miwili. Majirani wamesema  jamaa huyo amekuwa akimshambulia mkewe kila mara  na wakati mwingi marehemu alikuwa akitoroka kuokoa maisha yake .

Kamanda wa polisi wa kunti ndogo ya Isiolo George Kariuki  amesema  mshukiwa alizuiliwa katika seli mara moja  na mwili wa mkewe umepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Isiolo. Mkuu huyo wa polisi  amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo ili kutambua kilichosbabisha mauaji hayo .