Upekuzi: Fahamu kwa nini Moses Kuria yu mashakani

unnamed-compressed
unnamed-compressed

Makala ya upekuzi yamebaini kuwa ngome ya mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria umetekwa nyara na mahasimu wake wa kisiasa.

Upekuzi unaonyesha kwamba gavana wa zamani pamoja na mbunge mmoja wa zamani wanapanga njama za kuandamana juma lijalo dhidi ya Kuria ambaye kulingana nao, Kuria 'amepuuza mwelekeo wa Rais Uhuru Kenyatta.'

Hii ni njia mojawapo ya kupigia kampeni na kumteua kiongozi mwingine kutoka familia yenye ushawishi zaidi, kumbandua na kushika hatamu za uongozi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Haya yanatokea huku tofauti zikiibuka kutoka mirengo ya wanasiasa ikiibuka baina ya wanaunga mkono ripoti ya BBI huku wengine wakipinga.

Je, hii inaweza kuwa chanzo cha Moses Kuria kumpigia debe naibu wa Rais William Ruto ?