kate-actress-1

Upendo wa mama! Soma ujumbe wa Kate Actress kwa mwanawe

Kate Actress ni binti anayejivunia sana mtoto wake wa kwanza na ana furaha sana kwani mtoto wake amekuwa mkubwa na kwa sasa anafanya mtihani wa KCPE.
Kidosho huyu ana furaha mpitompwito na haamini vile ambavyo wakati umeenda mbio kwani ni juzi tu alikuwa anakazana kumlea mtoto wake akiwa mchanga sana na sasa amefika umri wa kuufanya mtihani wa kitaifa.

Nilipiga mpenzi wa mume wangu na alikuwa mja mzito – Joyce

Kate aliandika ujumbe mtamu kwenye mtandao wa kijamii na kumtakia mtoto wake heri njema anapofanya mtihani wake wa KCPE na kuzidi kusema kuwa Mungu atabariki kazi ya mikono yake.

”Ati nina mimba?” Betty Kyallo afunguka kuhusu uja uzito

Aisee! chanda chema huvishwa pete.

 ”I am so emotional right now my little Egg how did you get here? Thank you, Lord, 🙏🏿❤️Wishing all the Best to all KCPE candidates this year! God will reward your hard work”

Zaidi ya hayo, Kate aliweka ujumbe wa mzazi mwingine kwenye mtandao wa kijamii uliowaomba wazazi wao wazidi kuwapa watoto wao imani na kuwatia moyo wakati huu wa mtihani.

” Parents to the candidates I know our stomachs are running today but please remember your child’s well being and sanity is more important than their grades. That been said, let us be their peace and encourage them”

Kutoka Radio Jambo,tunawatakia wanafunzi wote wanaofanya mtihani wa kitaifa mwaka huu kila la heri katika mitihani yao.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments