Urembo na Uhondo wa Kupindukia:Kate amezaa kweli?

  Muigizaji  Catherine Kamau  maarufu  kama   Kate Actress  amekuwa akipinga sana  jitihada za kujirejeshea  makali ya kiurembo hasa baada ya kujifungua  Disemba mwaka jana .

Lakini Kate ana muonekano wa kipekee! Anapendeza kweli na picha zake anazotundika kwenye mitandao ya kijamii zinawaacha wengi  vinjwa wazi huku walio na jicho wakijiuliza kama kweli alipata mtoto. Kate ana bahati kweli kwa sababu baada ya kupata mtoto wa kike, mumewe  Phil Karanja alimnunulia bonge la zawadi-gari jipya na safi la  BMW X1.

Yote hayo kwa sababu tu ya kujifungua  mtoto..dah mambo hayo kweli ! Picha za Kate  kwenye ukurasa wake zina mvuto wa kipekee na  kidosho huyo anapendeza..Zitazame baadhi yazo…