Vanessa Mdee afichua kwamba anamatatizo ya macho

vanessamdeeandjumaincoast
vanessamdeeandjumaincoast
Mwanamziki kutoka Tanzania, Vanessa Mdee amefichua wazi kwamba jicho moja lake limekuwa na matatizo ya kuona vyema.

Vanessa alisema jambo hilo kwenye shoo ya pili ya 'East Africa Got Talent'.

Jambo hilo lilitokea baada ya mmoja kati ya wasanii wanaowania nafasi za raudi ya pili kuutetemesha umati. Msanii huyo ambaye yeye akizaliwa akiwa na tatizo hilo la Jicho pia alieleza kuwa aliwahi kuugua ugonjwa wa saratani katika maisha yake. Vanessa alimtia moyo kwa kumwambia asikufe moyo.

Vanessa alizidi kumpa moyo kijana huyo kwa kusema kuwa licha ya hali yake hio, jambo hilo halikumzuia katika kufuata na hata kutimiza ndoto zake.

"Sio jambo la kawaida kwa mtu mchanga namna hio kuimba wimbo mtamu vile tena mwenye hisia chungu nzima. Mie Mwenyewe nina tatizo la jicho kiasi fulani ila jambo hilo halikunizuia kutimiza ndoto zangu."

"Kwangu mie wewe ni mshindi licha ya matokeo ya mashindano haya. Usikufe moyo na uzidi kutia bidii kwani kwangu wewe ni mshindi."