(+ Video) Diamond Platnumz adondosha ngoma mpya na Teni wa Nigeria

Screenshot_from_2019_11_27_13_43_24__1574851436_82278
Screenshot_from_2019_11_27_13_43_24__1574851436_82278
Staa mkubwa Afrika Diamond Platnumz amedondosha nyimbo mpya Sound.

Wimbo huu wa dakika tatu na dakika thelathini na nne umetoka baada ya Baba Lao kufanya vizuri katika mtandao wa YouTube.

Midundo ya ngoma ya Baba Lao ulizua mushkil baada ya kufanana na ngoma ya Naira kutoka Nigeria.

Katika ngoma ya Sound, Diamond amemshirikisha Teni wa Nigeria.

Wimbo huu unatoka siku chache baada ya shirika la habari la CNN kumuorodhesha Diamond kama msanii mkubwa Afrika.

Diamond amekuwa katika mstari wa kwanza kuupeleka muziki wa Afrika katika levo za kimataifa.

Kando na kuwa msanii, Simba ana mchango mkubwa sana katika jamii.

Lebo ya WCB imeweza kuwasimamia wasanii wengi na kuwafanya mastaa wakubwa Afrika Mashariki.

Wasanii hawa ni Rayvanny, Mbosso, Dadake Queen Darleen, Lava Lava.

Rich Mavoko na Harmonize walikuwa mastaa katika lebo hii na baadae kuitema na kushughulika na muziki wao.

Audio ya Sound imefanywa na Lizer kutoka WCB huku kichupa cha video kikitendewa haki na Kenny (Zoom production) na Moe Mussa kutoka Nigeria.

Itazame hapa: