(+Video) Harmonize alivyomfurahisha Pombe Magufuli, dili na Wizkid

71789172_1377106175792116_1515609236131538878_n
71789172_1377106175792116_1515609236131538878_n
Nyota wa Bongo Fleva, Harmonize amewafurahisha maafisa za ngazi za juu serikalini kwa kuimba wimbo wa 'Magufuli.'

Katika wimbo huu, Harmonize anamsifia rais huyo pamoja na miundomisingi iliyojengwa na serikali ya sasa.

Konde Boy alikuwa anatumbuiza mashabiki na kuwakonga nafsi katika sherehe za Nyerere Day nchini humo.

Rais Pombe Magufuli hakusita kusimama na kusakata ngoma hii.

https://www.instagram.com/p/B3m-CFenJOo/

Hii ni baada ya wimbo huu kuwapendeza wengi katika hafla hiyo.

Haya yanajiri huku staa huyu akitangaza kufanya collabo kubwa na msanii kutoka Nigeria, Wizkid.

Konde Boy tayari ashatangaza kuibadili Bongo Fleva iwe na jina la Afro East ambalo anadhani linaafiki muziki huu ambao unatamba kwa kasi.

Jeshi alihakiki collabo hii kupitia mtandao wake maridhawa wa Insta.

Hafla hii ya AfroEast lilifanyika kwa siku 2 miji ya Melbourne, Sydney na nchini jirani ya Tanzania.

Kama Jeshi atamshirikisha Wizkid katika ngoma, hii bila shaka inatazamiwa kuwa kubwa zaidi baada ya kolabo na Yemi Alade, Burna Boy, Timaya na wengineo.