(+Video ) Kijana ‘ripota’ alamba dili nono Citizen TV, Mkurugenzi Joe Ageyo

Screenshot_from_2019_11_05_08_39_09__1572932386_65124
Screenshot_from_2019_11_05_08_39_09__1572932386_65124
Levis Saoli sasa ana nafasi kubwa na adimu ya kutangamana na wasomaji shupavu wa runinga ya Citizen.

Hii ni baada ya video fupi kuvuja akiripotia kituo hiki.

Mkurugenzi Joe Ageyo amefunguka kuwa Levis ana uhuru wa kufika na kutangamana studio hizo na wanahabari.

Alifunguka zaidi kuwa kijana huyu wa shule ya upili atapata mafunzo kutoka kwa wasomaji habari na kuwa kituo hiki kitamkuza ili kufikia kilele cha ndoto zake.

Soma hadithi nyingine:

"Kwa kweli tumevutiwa na kipaji chake na tunataka kuona uwezo wake. Tunampa mafunzo kwa sasa na anaruhusiwa kuingia studio zetu na kutangamana na wasomaji habari wetu..." Alisema Ageyo.

https://www.instagram.com/p/B4W4V46Avti/

Aidha, Saoli hataweza kupewa kazi kwa sasa mpaka amalize masomo yake na kusomea taaluma ya uanahabari.

"Hatuwezi tukamruhusu aripoti kwa sasa kwa kuwa bado ni mwanafunzi wa shule ya upili. Tunataka amalize masomo kwanza na achague iwapo atasoma taaluma ya uanahabari..." Alisema Ageyo.

Levis Saule alipata sifa kedekede katika mitandao ya kijamii baada ya kuripotia runinga ya Citizen.

Soma hadithi nyingine:

 Kijana huyu wa shule ya upili alionyesha talanta na ubunifu alionao.

Kipaza sauti alichoshika kilikuwa na nembo ya kujitengeneza ya Citizen TV.

https://twitter.com/LinusKaikai/status/1190552786339074048

Kilichovutia runinga ya Citizen ni ubunifu wa Levis,

Kijana huyu mara kwa mara alikuwa anashikashika sikio lake kuiga maripota wanavyofanya.

Taarifa yake aliyoiripoti ilisoma kama,

“Nimrod nakupata vyema, niko katika kaunti ya Narok ambapo shughuli ya kuwaondoa watu katika msitu wa Mau imefikia kikomo hivi leo. Shughuli yenyewe kulingana na kamishna wa Bonde la Ufa George Natembeya haijahusisha vurugu yoyote kati ya maafisa wa serikali na wanaoishi mle..” aliripoti Saule

Katika ujumbe wa Twitter, Linus Kaikai ambaye ni mkurugenzi wa stratejia na uvumbuzi katika kampuni ya Royal Media Services amefunguka kuwa wamepata kijana huyo.

“WE’VE GOT HIM!  has traced this talented secondary school student. Asanteni nyote.” Alichapisha Linus.