(+ Video) Kilichovutia Citizen TV kwa Levis Saule, alichoripoti

Screenshot_from_2019_11_03_10_14_45__1572765320_74063
Screenshot_from_2019_11_03_10_14_45__1572765320_74063
Mbunge wa eneo bunge la Ainabkoi ametoa tamko lake kuhusu Levis Saule .

Levis Saule alipata sifa kedekede katika mitandao ya kijamii baada ya kuripotia runinga ya Citizen.

Kijana huyu wa shule ya upili alionyesha talanta na ubunifu alionao.

Kipaza sauti alichoshika kilikuwa na nembo ya kujitengeneza ya Citizen TV.

https://www.instagram.com/p/B4W4V46Avti/

Kilichovutia runinga ya Citizen ni ubunifu wa Levis,

Kijana huyu mara kwa mara alikuwa anashikashika sikio lake kuiga maripota wanavyofanya.

Taarifa yake aliyoiripoti ilisoma kama,

"Nimrod nakupata vyema, niko katika kaunti ya Narok ambapo shughuli ya kuwaondoa watu katika msitu wa Mau imefikia kikomo hivi leo. Shughuli yenyewe kulingana na kamishna wa Bonde la Ufa George Natembeya haijahusisha vurugu yoyote kati ya maafisa wa serikali na wanaoishi mle.." aliripoti Saule

Katika ujumbe wa Twitter, Linus Kaikai ambaye ni mkurugenzi wa stratejia na uvumbuzi katika kampuni ya Royal Media Services amefunguka kuwa wamepata kijana huyo.

https://twitter.com/LinusKaikai/status/1190552786339074048

“WE’VE GOT HIM!  has traced this talented secondary school student. Asanteni nyote.” Alichapisha Linus.

Katika video hiyo,kijana huyu anaonekana akiripotia Nimrod Taabu akiwa maeneo ya Narok.

Anachoripoti ni shughuli ya kuwafurusha raia wanaoishi msitu wa Mau.

Serikali ina mipango ya kuhifadhi sehemu hii dhidi ya ukataji miti ovyo kutokana na mijengo na ukulima unaofanyika na raia.

Je, kuna uwezo Citizen TV ikamchukua kijana huyu na kumpa mafunzo zaidi?