(+Video ) Size 8 afunguka A-Z alivyopata presha akijifungua, video ya kinyonge

Screenshot_2019_11_19_at_10.53.13__1574319641_86943
Screenshot_2019_11_19_at_10.53.13__1574319641_86943
Nyota wa nyimbo za injili Size 8 amefunguka A-Z kuhusu mahangaiko yaliyomkumba akijifungua.

Muimbaji huyu alipata mtoto wake wa pili siku chache zilizopita.

Katika sherehe ya mtoto wake, size 8 alilia huku akiwaacha marafiki zake kusononeka zaidi na kumhurumia.

https://www.instagram.com/p/B5CYV6hggsB/

"Mtu yeyote asichukulie sherehe kama hizi kimzaha. Tujifunze kusema shukarani kwa chochote maishani. Kwangu mimi, kufika hapa ni muujiza tu. Nimenusurika kifo mara sio moja. Hata uwe na mabilioni ya hela huwezi kuwa na amani kabisa..."

Alielezea makali ya ujauzito miezi michache baada ya kuharibikiwa na mimba.

"Nilishtuka sana na nikauliza mume wangu(Dj Mo). Ule ujauzito mwingine uliharibika,je huu ukiharibika kutakwendaje? Kwa hiyo tukaenda hospitali na nikaanza kupata usaidizi..." Alisimulia.

https://www.instagram.com/p/B44tKQtFTn6/

"Wiki tatu nyuma nikawa na matatizo ya presha ya damu ila ikashuka chini baada ya muda mchache. Ghafla nikaanza kuhisi uchungu katika mfuko wa mtoto..."

Baadaye msanii huyu alichapisha video ya kinyonge sana akiwa hospitalini.

https://www.instagram.com/p/B5An0T1FH1i/

Video hii imewafanya mashabiki wake kumhurumia zaidi na kuahidi kumuombea.

Haya yanajiri baada ya Dj Mo na Size 8 kubarikiwa na mtoto.

Katika video hii, Size 8 anaonekana amekalia kitanda hospitalini huku mipira ikiwa bado kinywani.

Hali ya unyonge imewafanya mashabiki kutuma pole zao.