Video ya siku: Mesut Ozil awatuza mashabiki wa Arsenal kutoka Kenya

Miezi minane iliyopita, Mesut Ozil ambaye ni kiungo wa Arsenal, aliwafurahisha wakenya wote na watu wengi duniani baada ya kumtumia kijana kwa jina Lawrence pamoja na familia na marafiki zake sare za Arsenal zilizo na jina lake pamoja na viatu vya aina yake.

Hii ni kufuatia picha moja iliyochapishwa mtandaoni wa Twitter na mwanahabari kwa jina Njiiru, ikionesha Lawrence akiwa likizoni akilinda ng'ombe wao huku akiwa amevalia shati ya kujiundia iliyo na jina 'Ozil'.

Wakenya wote na wapenzi wa kadanda waliungana na kuhakikisha picha ile imemfikia Ozil. Na ilipomfikia, hakusita wala alihakikisha shabaki wake Lawrence na marafiki zake wamepata sababu ya kutabasamu.

https://twitter.com/MesutOzil1088/status/1105182652225777665?ref_src=twsrc%5Etfw%7Ctwcamp%5Etweetembed%7Ctwterm%5E1105182652225777665&ref_url=https%3A%2F%2Fradiojambo.co.ke%2Fmesut-ozil-wows-kenyans-after-sending-signed-jerseys-and-boots-to-young-herder%2F

Isitoshe, hapo jana Ozil alithibitisha upendo wake kwa Kenya na wakenya baada ya kuwatumia wanachama wa 'Arsenal Kenya' zawadi ya jezi yake aliyoipiga saini mwenyewe.

Wanachama hao hawakuficha furaha yao na waliimba nyimbo za kumsifu kiungo huyo aliyeshinda kombe la dunia na Germany mwaka wa 2014.

Kwa upande wake, Ozil hakusita kuwapongeza na alikuwa na maneno mema kwa mashabiki hao huku akifurahishwa na jinsi wanavyompenda na kumpa moyo kila siku.

Aliandika,

This support is overwhelming! ❤🙏🏼 I hope you will find a good place for my little gift 👍🏼😉 Thank you so much Kenya 🇰🇪 #M1Ö #YaGunnersYa