Viongozi wa mlima Kenya kuunda uongozi wa kuimarisha msaada

1892751
1892751
Viongozi kadhaa kutoka mlima Kenya wameunda kamati ya kuimimarisha msaada wa Uhuru Kenyatta katika mkoa huo.

Aliye teuliwa mbunge wa mlima Kenya Maina Kamanda, alisema kuwa agenda ya (Mt.Kenya Diaspora Leadership Forum) ni kumsaidia rais Uhuru kukamilisha agenda yake ya maendeleo ya taifa.

Jukwaa hilo limeingiza walio ndani na nje ya nafasi ya kuchaguliwa akiwemo waliokuwa wakiwania kiti cha urais Peter Kenneth na Martha Karua.

Mbunge wa Mathioya, Murang'a Peter Kimari  na mwenzake Ruth Mwaniki wamejiunga na Kikundi hicho.

Akiongea akiwa kanisa la Njau-ini ACC jumapili alisema kuwa kikundi hicho kitaenda katika mkoa huo kusajili wanachama wengi zaidi ili wajiunge na kikundi hicho.

Alisema kuwa ni jambo kubwa au la maana viongozi wa mitaanai kumsaidia rais kukamilisha maendeleo yake kabla ya muhula wake kuisha.

Pia aliweza kupendekeza kuwepo na kiti cha waziri mkuu katika kura ya mapendekezo,

"Wacha swali la kuingiza kiti cha waziri mkuu likuwe katika kura ya maoni, na tuwaache wananchi waamue ambacho wanataka," Alisema Kamanda.

Alisema kuwa kiti hichi kitamsaidia rais zaidi kuleta taifa pamoja na kupunguza vurugu zinazo fanyika kwa ajili ya uchaguzi, kwa maana mikoa mingi itakuwa katika serikali.

Hisia zake ziliungwa mkono na aliye kuwa mbunge wa Dagoretti south Dennis Waweru aliye sema jukwaa hilo la uongozi litasaidia kuleta pamoja viongozi wa mkoa.

"Awali wendi wetu tulijilikana kwa kuwaleta watu pamoja katika mkoa wa mlima kenya," Alizungumza Waweru.

KWINGINEKO NIKUWA:

Naibu mwenyekiti wa kamati ya kilimo katika bunge la kitaifa ambaye pia ni mbunge wa navakholo Emmanuel Wangwe amepuuzilia mbali madai kuwa serikali imetuma pesa ya wakulima wa miwa katika kiwanda cha sukari cha nzoia.

Wangwe amesema pesa za kuwalipa wakulima hazitatumwa kwenye kampuni za sukari bali moja kwa moja kwenye akaunti za wakulima.