Stori za Ghost: Jamaa aachwa baada ya mkewe kugundua ana nyumba ya nyasi kijijini ilhali wanaishi kifahari Nairobi

Muhtasari

•Mwanadada huyo alisikitika sana kuona hali duni ya nyumba ambayo jamaa amejenga pale kijijini ilhali walikuwa wakiishi maisha ya kifahari jijini Nairobi.

Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha 'Stori za Ghost' mtangazaji Ghost Mulee alisimulia kisa kimoja kilichohusisha wapenzi wawili ambao ndoa yao ya miaka mitatu ilisambaratika wakati jamaa alipeleka mkewe nyumbani kwao kwa mara ya kwanza.

Ghost alisimulia jinsi mwanadada alimshinikiza mumewe ampeleke nyumbani kwao upande wa Siaya na hatimaye akakubali na  wakaabiri ndege kuelekea kijijini ambako jamaa alizaliwa na kulelewa.

Mwanadada huyo alisikitika sana kuona hali duni ya nyumba ambayo jamaa amejenga pale kijijini ilhali walikuwa wakiishi maisha ya kifahari jijini Nairobi. 

"Jamaa amekuwa na mwanadada kwa miaka tatu. Wamekuwa wakiishi maisha ya kifahari na anaendesha kubwa.Nyumba yao imetengenezwa vizuri. Ni jamaa ambaye ana mazoea ya kujigamba wanapoenda mahali. Mpenzi wake alimwambia wamekuwa wakiishi Nairobi kwa kipindi kirefu  na angependa waende kijijini. Waliingia kwa ndege na wakafika. Kufika kijijini Siaya mwanadada alishtuka sana. Jamaa ananyumba ya nyasi hajajenga. Mwanadada alipoamka asubuhi alimwambia kuwa mapenzi yao yameisha"  Ghost alisimulia.

"Mwanzoni mwanadada alidhani ni mzaha lakini alipoamka asubuhi jamaa akamwambia kuwa hapo ndipo nyumbani ila anapanga kujenga. likuwa mara ya kwanza kupelekwa Siaya. Alisema  haiwezekani wanaishi maisha ya kifahari Nairobi ilhali kijijini hajajenga. Hapo na hapo akaambia jamaa mapenzi yao yameisha na kila mtu akarudi Nairobi kivyake" Alisimulia Ghost.