Jacob 'Ghost' Mulee afichua kwa nini aliacha kushabikia Arsenal licha ya kula lunch na Arsene Wenger

Alisema katika siku ambazo aliwasapoti wanabunduki, hata alikula pamoja na kocha wa zamani Arsene Wenger.

Muhtasari

•Ghost alisema aliacha kuwaunga mkono wanabunduki  baada ya kugundua kwamba hawakuwa wakishinda chochote.

•Gidi alimkosoa kwa uamuzi wake wa kuacha kushabikia Arsenal, akisema kama vile katika ndoa, alipaswa kuvumilia.

Aliyekuwa kocha wa Harambee Stars, Jacob 'Ghost' Mulee

Mtangazaji mcheshi wa kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kwenye Radio Jambo, Jacob ‘Ghost’ Mulee amefichua kuwa wakati mmoja alikuwa shabiki wa Arsenal.

Katika mahojiano ya kipekee na Radio Jambo, kocha huyo wa zamani wa Harambee Stars alisema aliacha kuwaunga mkono wanabunduki  baada ya kugundua kwamba hawakuwa wakishinda chochote.

Alisema alilazimika kuacha kuwa mwaminifu kwa klabu hiyo ya  EPL kwani alikuwa na wasiwasi kwamba msongo wa mawazo ungemuua.

“Nilikuwa shabiki wa Arsenal. Nilisapoti Arsenal. Lakini ile kitu iliacha niache kusupport Arsenal, ningeshakuwa nimekufa saa hii. Shinikizo, hawashindi! Walikuwa wanasema msimu ujao, msimu ujao. Mpaka saa hii, ni msimu ujao” Ghost Mulee alisema.

Aliendelea kufichua kwamba katika siku ambazo aliwasapoti wanabunduki, hata alikula pamoja na kocha wa zamani Arsene Wenger.

"Nimekula lunch na Arsene Wenger huko Highbury. Hiyo ilikuwa mwaka wa 2003. Wakati tulikula lunch na yeye, kipindi hicho Ribbery alikuwa anafanya regeneration,” alisema.

Baada ya kuacha kuishabikia Arsenal, kocha huyo wa zamani wa Harambee Stars alianza kuisapoti Manchester United ambayo pia imekuwa haifanyi vyema hivi majuzi.

Mtangazaji mwenzake, Gidi Gidi alimkosoa kwa uamuzi wake wa kuacha uaminifu wake kwa Arsenal, akisema kwamba kama vile katika ndoa, alipaswa kuvumilia.

“Bado upo kwenye ndoa? Kama ndoa haijafanya ukawa na pressure, sasa Arsenal ni kitu itakusumbua?” Gidi alimuuliza.

Gidi kwa upande wake alisema amekuwa mwaminifu kwa Arsenal kwa zaidi ya miongo mitatu.

Alisisitiza uaminifu wake, akiashiria kwamba pia amekuwa akiunga mkono wachezaji wake wanaopenda.

“Mimi ni mwaminifu kwa Arsenal tangu wakati nilianza. Mimi pia ni shabiki wa Lionel Messi tangu wakati huo, na Freddie Ljungberg, pamoja na Thiery Henry, ni wachezaji niwapendao wakati wote. Sasa hivi pale Arsenal , Odegaard, mtu wangu na  Rice,” Gidi alisema.

Mwimbaji huyo wa zamani wa kundi la ‘Gidi Gid Maji Maji’ alisema kuwa wanaume ni viumbe waaminifu, akidai kuwa ni waaminifu kwa klabu zao za soka, vinyozi na ndoa.

"Kitu kimoja kuhusu wanaume ambacho watu wanafaa kujua, mara unapoamua juu ya jambo fulani, hasa mambo ya mpira ata kinyozi, na hata mambo ya ndoa, basi ameamua," Gidi alisema.

Pia alifichua kuwa kinyozi aliyeanza kumnyoa akiwa shule ya upili bado anamnyoa hadi leo, na hajawahi kubadilika tangu wakati huo.

“Mimi kwa mfano saa hizi, kinyozi alianza kuninyoa nikiwa highschool ndiye ananinya mpaka leo. Huwa anahama, alianza na town, akaenda Hurlingam, anaenda wapi, lakini mimi humfuata hadi leo, Huyo ni kinyozi wangu mpaka leo, uaminifu,” alisema.

Mtangazaji huyo mahiri alidai kuwa wanaume sio watu wasio waaminifu bali ni wanawake ambao huzua usumbufu.