Nuru Okanga ataja sababu mbili kuu za kufanya KCPE akiwa na miaka 32

Hata hivyo alisusia kuweza wazi alama zake za mtihani huo,huku akisimulia furaha aliyonayo kwa kupata alama zinazoenea mitandaoni.

Muhtasari

• Katika mazungumzo na mtangazaji Massawe Japanni katika stesheni ya Radio Jambo kwenye kitengo cha Ilikuaje, ,Okanga alisema kuwa sababu ya kwanza ya kufanya  mitihani hiyo ni kutaka kupata cheki 

• “Sababu ya kwanza,niko na nia ya kuwania kiti cha uwakilishi wodi,ndio maana niliamua kutafuta cheti, pili sitaki kuwa mwanasiasa ambaye hana vyeti,”

Nuru Okanga
Nuru Okanga
Image: FACEBOOK

Mfuasi  maarufu wa   chama azimio nuru Okanga,amejitokeza wazi na kueleza sababu zilizompelekea kufanya mitihani ya KCPE mwaka huu licha ya umri wake.

Katika mazungumzo na mtangazaji Massawe Japanni katika stesheni ya Radio Jambo kwenye kitengo cha Ilikuaje, ,Okanga alisema kuwa sababu ya kwanza ya kufanya  mitihani hiyo ni kutaka kupata cheki  kitakachomsaidia kuwania kiti cha uwakilishi wodi.

Alisema sababu za pili ni kuwa yeye hataki kuwa mwanasiasa ambaye hataongoza bila makaratasi ya kudhibitisha amefuzu.

“Sababu ya kwanza,niko na nia ya kuwania kiti cha uwakilishi wodi,ndio maana niliamua kutafuta cheti, pili sitaki kuwa mwanasiasa ambaye hana vyeti,”alisema.

Hata hivyo alisusia kuweza wazi alama zake za mtihani huo,huku akisimulia furaha aliyonayo kwa kupata alama zinazoenea mitandaoni.

Okanga ametaja nia yake ya kujiunga na shule ya sekondari ya alliance,akitaja kwa furaha jinsi mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino amejitolea kumfadhili ili kukamilisha masomo yake ya sekondari.

Nuru amesimulia hali ngumu aliyopitia wakati akikuwa amabyo anadai ilichangia yeye kuacha shule na kufanya kazi ndogondogo kujikimu kimaisha.

Okanga mwenye umri wa miaka 32 alisema kwamba kilichofanya hakusoma mapema akiwa mdogo ni kutokana na kifo cha babake.

Alisema babake alifariki yeye akiwa na miaka 6 tu na yule ambaye aliachiwa majukumu ya kuwalea na kuwasomesha alikwepa na hapo ndipo aliacha shule ili kujukumikia familia.

“Niliacha shule nikaanza kuchunga ng’ombe, nilikuwa nalipwa shilingi elfu moja na baadae elfu 3 na kisha nikaamia ukambani sehemu inaitwa Konza kuchunga kondoo, huko nilikuwa nafanyia 8,500. Nikaona huu ni upuzi nikaachana na hiyo kazi nikakuja hapa Nairobi. Nilianza kuchunga ng’ombe nikiwa na miaka 10. Nilitoka ukambani 2013 na nikakuja Nairobi nikaanza kufanya mjengo,” Okanga alisema.