Patanisho:Mwanadada agura ndoa baada ya kuzozana na shemejiye aliyeita mwizi kwa kufanikiwa sana kifedha

Muhtasari

•Manyasi alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka mitatu na kumuachia watoto wao wawili wakati alitofautiana na dada yake mmoja ambaye alifikiwa na fitina ambazo alikuwa ameeneza dhidi yake.

•Alifichua kwamba mkewe alikuwa ameanza kueneza uvumi kuwa alimpigia simu akitishia kujitoa uhai juu ya kuachwa, madai ambayo alipuuzilia mbali.

Ghost na Gidi
Ghost na Gidi
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho jamaa aliyejitambulisha kama Alex Manyasi (30) kutoka Kitale alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Maureen Moraa (24)  ambaye aliondoka nyumbani miezi mitatu iliyopita baada ya kuzozana na dada yake.

Manyasi alisema mkewe aligura ndoa yao ya miaka mitatu na kumuachia watoto wao wawili wakati alitofautiana na dada yake mmoja ambaye alifikiwa na fitina ambazo alikuwa ameeneza dhidi yake.

Alisema mkewe alishirikiana na dada yake mmoja kueneza fitina dhidi  ya dada yake mwingine ambaye amefanikiwa sana kihela kwamba ni mwizi. Aliyekuwa anaongelewa alifikiwa na fitina hizo akakabiliana naye kumuuliza ndiposa wakakosana

"Dada ambaye walikuwa wanaongelea amenisaidia sana. Niliona mke wangu alimuongelea mambo mengi singemtetea. Nilipata ajali mwaka wa 2019 na dada ambaye waliongelea alinisaidia sana akalipa bili ya hospitali kwa hivyo nilishindwa nifanye vipi. 

Walisema eti dadangu amekuwa mwizi. Kwa hii boma yetu yeye ndiye husaidia kila mtu, yeyote akiwa na shida anamsaidia. Walisema labda pesa yake yote ni ya wizi. Kuanzia 2019 mimi sifanyi kazi, nikiwa na shida dadangu hunisaidia. Nashindwa nitaanza vipi kukosana naye" Manyasi alisema.

Alisema licha ya yote angependa mke wake arudi nyumbani ili waendelee kulea watoto wao wawili.

Juhudi za kuwasiliana na Bi Moraa ziliangulia patupu licha ya Gidi kwani alisita kuchua simu licha ya Gidi kumpigia mara tatu.

Manyasi alifichua kwamba Moraa alikuwa ameanza kueneza uvumi kuwa alimpigia simu akitishia kujitoa uhai juu ya kuachwa, madai ambayo alipuuzilia mbali.

"Ametangazia kila mtu, mama yangu na pia dada yangu mwingine eti nataka kunywa simu na watoto. Hata sijafikiria kitu kama hichokabisa. Nilimwambia harudi hataki kurudi. Sikumpigia simu eti nataka kunywa simu na watoto, sijui alitoa maneno hayo wapi"  Alisema.

Manyasi alimhakikishia mkewe kwamba hana ugomvi wowote naye huku akiahidi kuzungumza na dadake ili wasameheane.

Pia alimfahamisha kuwa hana mpango wa kunywa simu pamoja na watoto wao