Mwanaume amfukuza mkewe kwa kuwa na uhusiano na kakake

Martha alisema kuwa walikosana na Newton kwasababu alidhani kuwa yeye ako na uhusiano wa kimapenzi na ndungu yake Brian ambaye alikuwa anakaa nao wakati huo.

Muhtasari
  • Newtone alipigiwa simu akasema kuwa  bibi yake alikosea na pia yeye anajua kwa hivyo ataita wazazi ili watatue hiyo shida yote.
GHOST NA GIDI STUDIONI
GHOST NA GIDI STUDIONI GHOST NA GIDI STUDIONI
Image: RADIO JAMBO

Martha Grace kutoka Kitui alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na bwanake Newton ambaye alikosana naye juu ya vitu ndogo ndogo.

Martha alisema kuwa walikosana na Newton kwasababu alidhani kuwa yeye ako na uhusiano wa kimapenzi na ndungu yake Brian ambaye alikuwa anakaa nao wakati huo.

Newtone alianza kushuka Martha na Brian, Martha akachukua vitu zake na kuenda kwao. Aliporudi  kwa bwanake,  alimpata na mke mwingine.

“Tulianza kuchumbiana mwaka wa 2022 na baada ya miezi kadhaa nikaanza kuishi na yeye. Ndungu yake Briana akaja akaanza kuishi na sisi na kisha baada ya muda fulani bwanangu akaanza kushuku kuwa niko na uhusiano wa mapenzi na ndungu yake me nikakasirika nikaenda kwetu na  wakati niliporudi nilimpata na mwanamke mwingine”, Martha alielezea Gidi na Ghost.

Martha na Newtone bado walikuwa wakiongea kwa simu na Newtone huku akikiri kuwa bado anampenda Martha na hapendi huyo mwanamke ako na yeye kwa nyumba.

“Tumekuwa tukiongea kwa simu na ananiambia kuwa hapendi huyo mwanamke mwingine, ni mimi anapenda na anataka nirudi”, Martha alisema

Martha alipoulizwa kama ni ukweli walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Brayo , alijibu kuwa, “Ndungu yake alishinda akiniambia kuwa huwa anampata na wanawake tofauti pahali anafanya kazi”.

Newtone alipigiwa simu akasema kuwa  bibi yake alikosea na pia yeye anajua kwa hivyo ataita wazazi ili watatue hiyo shida yote.

“Si wewe unajua ulikosea, hizo mambo tutaongea baadaye na tutaita wazazi watatue hii mambo”, Newtone aliambia bibi yake Martha.

Newtone alieleza sababu yake kumfukuza Martha ni kuwa alikuwa anatembea na marafiki zake na hakupenda hiyo tabia.

Aliendeleza kusema kuwa alikuwa anaskia ati Martha alikuwa anamtembelea ndungu ya bwana yake.

“Alikuwa anatembelea Brayo kwake kila wakati na huyo ndungu yangu pia ako na bibi”.

Martha alijitetea kuwa Brian alimwita amtembelee na hakuna kitu ambacho kilitendeka kati yao.

“Brayo aliniita niende nimtembelee na hakuna kitu ambacho  kilifanyika kati yetu. Brayo alikuwa na bibi kwa hivyo hakuna kitu kilichokuwa kikiendelea”.

Ghost alimuuliza Martha kama wakati alienda kutembelea Brayo kama bibi yake alikuwa kwa nyumba, Martha akajibu kuwa bibi yake hakuwemo.

Newtone alieleza kuwa angalau mke wake angemwambia kuwa anaenda kumtembelea Brayo lakini kitendo cha kumfichia taarifa hiyo kilimkasirisha na kumfanya amfukuze Martha.

Newtone na Matha waliambiwa waambiane maneno ya mwisho na Martha alionyesha upendo wake kwa Newtone huku Newtone akitaka mkewe  kubadilisha mienendo yake.

“Newtone ni wewe ndio napenda. Hakuna mtu yeyote ni nanaye penda”, Martha alikiri.

“Martha kama tutarudiana itabidi umerekebisha tabia tabia yako na ni lazima tuone wazazi kwanza ndio tujue baada ya hapo”, Newtone alisema.