Vituko vya Virginity! Mambo wanayofanya na bidhaa wanazotumia wanawake ili kujirejeshea ‘Ubikra’ – Maajabu!

Kuna vitu vya kustaajabisha ambavyo wanawake  hutumia ili kurejesha ubikra wao  na masimulizi ya jinsi vinavyotumiwa yatakuacha kinywa wazi.

Kuna mjadala usiopitwa na muda wa mbona wanawake hutaka kuendelea kujiuza kama walio bikra lakini hilo ni la tangia jadi kwamba hakuna mwanamme anayateka kwenda na mwanamke aliyevunja ubikra zamani.

Ndimu

Kama hukujua, wajuzi inadaiwa wanawashauri wanawake wanaotaka ‘kujirejeshea’ ubikra kujikamulia ndimu katika sehemu zao za uke ili kubana tena sehemu hizo kwa kiasi cha kuweza kutambulika kama mabikra. Kando na uchungu wa ndimu au limau, sitaki kujiingiza katika mjadala kuhusu  uchungu wa jusi ya ndimu katika ngozi ya ndani.

Yoghurt

Kinywaji  ambacho hakina hatia kilichoundwa kwa maziwa, sasa kimepata kazi isiyokuwa ya kawaida. Yadaiwa kwamba utumizi wa kinywaji hiki katika sehemu husika ni hatua inayoweza kukurejeshea ubikra.

Coke

Kufikia sasa, orodha ya vinavyotumiwa kurejesha ubikra najua imeanza kukuhofisha lakini katika orodha hii pia yadaiwa soda hii ya Coke pia hutumiwa na baadhi ya wanawake ili kubana sehemu zao kwa lengo la kurejesha ubikra wao.  Huwezi kuanza kufikiria kuhusu  ujuzi wa kununua Coke dukani kwa lengo la kujibana uke. Walioanzisha kinywaji hiki najua watashangaa kugundua kinavyotumiwa badala ya kukata kiu.

 Matufe ya Barafu/Ice Cubes

Wanaofahamu  uzuri na  barafu katika kinywaji unachokipenda wanajua jinsi kinavyoweza kukutuliza koo. Lakini wajuzi sasa wanajipa raha ra baridi ya barafu ili kujirejeshea ubikra. Yamkini baadhi ya ushauri huu unaotolewa unazua maswali kuhusu  kituo hicho cha utafiti ambacho kilifanya yote haya kwa siri na kugundua matumizi mbadala ya  barafu .

Krimu, kemikali, sprei

Jijini Nairobi,  kuna  vitovu kwa yote haya, krimu za kuweza kujipaka na kujipata umekuwa bikra katika kipindi kama cha wiki tatu. Eneo la River Road  ni  ngome ya yote haya na mwanamke akiwa na tatizo lolote kuanzia kutaka kubana sehemu yake ya uke ili kuwa bikra kama msichana mdogo hadi kuboresha ungo na umbo kama tausi – kuna kila aina ya kemikali au tembe zinazotumiwa.

Mazungumzo na wanaouza ‘mazuri’ yote  hayo yatakufichulia mengi ambayo kando na kukushangaza, pia yatakupa tabasamu na pia kukukarishia hofu. Liz, mmoja wa wauzaji wa bidhaa hizo  anasema kuna vijiwe vinavyoyeyuka ambavyo vinauzwa kwa shilingi 350. Unavibondabonda kisha unavichanganya na maji ya kuoga  na kisha kujipanguza kwa kitambaa katika sehemu yako ya uke  halafu  muujiza wa ubikra utaonekana baada ya muda usiokuwa mrefu. Liz anasema kuna tembe za kiasili ambazo pia zinaweza kukusaidi kuzidisha ukubwa wa makalio na zinauzwa kwa shilingi 6,500.

Rose, muuzaji mwingine  anasema kuna tembe unazohitaji kumeza kama kumi kwa siku tano ili kufanya mambo kuwa mazuri ‘pale chini’.