Vurugu zashuhudiwa katika bunge la kaunti ya Kitui wakati wa kujadiliwa kwa mswada wa kumtimua gavana

ngiluu
ngiluu
Vihoja vimeshuhudiwa mapema hii leo katika bunge la kaunti ya Kitui baada ya mawakili wanaomwakilisha gavana Charity Ngilu kutimuliwa na wawakilishi wadi wa kaunti hiyo.

Mapema hii leo, mawakili hao walikuwa wamezuiliwa kuingia katika bunge hilo hatua ambayo waliitaja kuwa kinyume na sheria.

“You cannot lock us out of a public office, huku si kwa mamayako ama babayako, tell the speaker to give us as letter of cancellation, you invited us, no one is getting into this office if you do not allow us in,” Wakili Morris Kimuli .

Kulinmgana na mawakili hao, walikuwa wameenda katika bunge hilo kumwakilisha gavana ambaye alikuwa ameagizwa kufika mbele yake.

MCAs walikuwa wamemtaka Ngilu kufika mbele ya bunge hilo siku chache tu baada ya mahakam ya kuu kusitisha mchakato wa kutimuliwa.

Mawakili hao Morris Kimuli na Martin Oloo walikuwa wamejihami na faili za ushahidi huku taarifa zikidai kuwa Kimuli alijeruhiwa wakati wa vurugu hizo.

Wakili huyo sasa yuko katika hospitali kuu ya Kitui huku mwenzake akilazimika kuandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Kitui.