Vyama vya Kalonzo, Rutto vyasiani mkataba wa Kujiunga na Jubilee

Vyama vya Wiper  na  CCM  vimesaini mkataba wa  ushirikiano na chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta .

Kiongozi wa Wiper  Kalonzo Musyoka na gavana wa zamani wa Bomet  Isaac Rutto  walikuwa katika hafla  hiyo katika makao makuu ya chama cha Jubilee . Katibu mkuu wa chama cha   Judith Sijeny  amesema lengo lao kujiunga na Jubilee kupitia makubaliano hayo ya ushirikiano   ni kuwaleta watu pamoja . Mwezi uliopita  baraza kuu la usimamizi wa chama cha Wiper Lilimpa kalonzo Idhini ya kusainia makubaliano ya kushirikiana  na Jubilee . Mwafaka uliafikiwa baada ya mkutano uliofanywa kupitia njia ya video na zaidi ya watu 50

Wanachama hao  waliunga mkono kwa kauli moja kutekelezwa  kwa mkataba huo wa ushirikiano huo. Wakati wa mkutano huo  Kalonzo amesema makubaliano hayo  haumaanishi kwamba wamejiondoa kutoka  muungano wa NASA .

Mkataba huo  unajiri  baada ya chama cha Kanu pia  kusaini mkataba   wa ushirikiano nan a Jubilee. Mkataba huo wa Kanu na Jubilee ulifanikisha kuteuliwa  kwa seneta wa West Pokot Samuel Poghisio wa  Kanu  kutajwa kuwa kiongozi wa walio wengi katika senate .

Mwezi ulipita Rutto  alifichua kwamba  alikuwa akijadili mkataba wa ushirikiano  wa kisiasa na rais Uhuru Kenyatta .Rutto ni mshirika wa karibu wa seneta wa Baringo   Gideon Moi  ambaye pia chama chake cha KANU kipo katika makubaliano ya kisiasa na Jubilee .