Waafrika si panya wa kufanyiwa majaribio ya chanjo ya Corona! Eto'o'na Drogba wasema

vaccine
vaccine
NA NICKSON TOSI

Baada ya video  kuenea katika mitandao ya kijamii ikionyesha wanasayansi wawili wa Ufaransa wakijadiliana kuhusiana na hatua ya kufanya majaribio ya chanjo ya virusi vya Corona kwa miili ya Waafrika, watu wengi kutoka bara hili la Afrika wamejitokeza na kuwakashifu wanasayansi hao kwa usemi huo .

Miongoni mwa watu waliogadhabishwa na usemi wa madaktari hao, ni wachezaji wa kitambo wa timu za taifa la Cameroon na Ivory coast Didier Drogba na Samuel Eto'o ambao wametaja usemi huo kuwa upuzi na usiostahiki katika karne ya sasa.

Usemi wa wanasayansi hao Sean Paul Mira na mwenzake unajiri wakati taifa la Ufaransa limesajili vifo vya watu wengi zaidi ikilinganishwa na idadi ya vifo ambavyo vimesajiliwa  katika bara la Afrika .

Kwa sasa, Italia inaongoza na vifo 14,009, Uhispania 10,935 , Amerika 6,099 kisha Ufaransa na Uchina zikifuata mtawalia huko bara la Afrika likiwa ndilo lililosajili vifo vya watu vichache zaidi.