image-2019-03-11-4-1

Waathiriwa wa ajali ya ndege hawatawahi patikana – CEO Ethiopian Airlines

Ni kilio ambacho jamii za waathiriwa wa ajali ya ndege ya Ethiopian ET 302 iliyoanguka baada ya kuong’o nanga wanalia mioyoni mwao na huzuni ambao wanao, kwa kuto pata mili ya watu wao katika tukio la ajali hiyo.

Ni majivu tu na baadhi ya viungo vya mili yao ambavyo vimesalia kama ukumbusho wa wana jamii, jana jamaa zao waliweza kufika katika tukio la ajali hiyo lakini matumaini yao yaliambulia patupu.

Ahmed Khalid alikosa kusafiri na ndege ya Ethiopian iliyofanya ajali

53320153_419773955259491_2899677319877867493_n(2)

Baadhi ya mili ya watu 157 wakiwemo wakenya 32, waliohusika kwa ajali hiyo haitawahi onekana wala kutambulikana na hata kuzikwa kwa sababu waathiriwa hao waliweza kuchomeka hadi kuwa majivu.

Katika mahojiano kwa runinga ta BBC na CEO wa Ethiopian Airline, Tewolde Gebremariam aliweka wazi kuwa mili mingi ilichomeka na moto na baadhi ya viungo ndivyo vimeweza kupatikana.

0_People.walk.at.the.scene.of.the.Flight.ET.302.plane.crash.near.the.town.of.Bishoftu

“Wakati nilipowasili katika tukio la ajali, ndege ilikuwa kabisa chini ya ardhi na hakukua na ishara ya ndege hiyo ardhini,

“Ilitubidi tuanze kuchimba ili kutoa mabaki ya ndege hiyo na tukaanza kutafuta mili ya waathiriwa,

“Ni jambo la kuhuzunisha kuwa hatukuweza kupata mili yeyote, tumeweza kupata baadhi ya viungo ambavyo ni vidogo sana,

“Hiyo ndiyo changamoto ambayo tuko nayo kwa sasa.” Alieleza CEO Tewolde.

R.I.P: Familia kuomboleza kifo cha rubani wa ndege ya Ethiopian Yared

Cedric Asiavugwa ambaye alikuwa miongoni mwa waathiriwa hao, alikuwa anaishi Washington DC na alikuwa amekuja katika  mazishi ya mama mkwe wake.

Cedric Asiavugwa
Mwenda zakeCedric Asiavugwa

Baba yake Thomas Govedi akiongea katika mahojiano na stesheni moja nchini alisema kuwa alizidiwa na habari hizo za kuhuzunisha,  lakini aliongeza na kusema hatakama ni kidole ambacho watapata wataweza kukizika.

“Ata kama ni kidole tutapata tutakizika.” Aliongea Timothy.

Cedric ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Georgetown na ambaye alikuwa anasimea sheria, alikuwa aweze kuhitimu baada ya miezi miwili.

Ujumbe wake wa mwisho aliandikia mke wake akimpa faraja kwa kumpoteza mama yake, ufuatao ni ujumbe ambao alimtumia mke wake.

“THE GREAT AND SAD MISTAKE OF MANY PEOPLE — AMONG THEM EVEN PIOUS PERSONS — IS TO IMAGINE THAT THOSE WHOM DEATH HAS TAKEN, LEAVE US.

THEY DO NOT LEAVE US. THEY REMAIN! WHERE ARE THEY? IN DARKNESS? OH NO! IT IS WE WHO ARE IN DARKNESS.

WE DO NOT SEE THEM, BUT THEY SEE US. THEIR EYES, RADIANT WITH GLORY, ARE FIXED UPON OUR EYES . . .

OH, INFINITE CONSOLATION! THOUGH INVISIBLE TO US, OUR DEAD ARE NOT ABSENT. THEY ARE LIVING NEAR US, TRANSFIGURED INTO LIGHT, INTO POWER, INTO LOVE.” Aliandika.

 

 

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments